CLARA MALINGUMU

Kinara

About CLARA MALINGUMU

Naitwa Clara prosper,ni mzaliwa wa kwanza kwenye familia ya watoto watatu wa Mr&Mrs prosper malingumu ,ambao kwa sasa ni marehemu.Baada ya wazazi wangu kufariki sikuweza kuendelea na shule,niliishia kidato cha tatu kutokana na kukosa mtu wa kunisomesha,hivyo nilikaa nyumbani kwa aunt yangu,lakini nilifanya kila jitihada kuhakikisha wadogo zangu wawili ambao ni wa kiume wanasoma.nikiwa na Umri wa miaka 17 nilitolewa posa nikaolewa na mwanaume aliyenioa ni dereva wa malori na baada ya kuolewa nilipata changamoto nyingi za maisha hali iliyonifanya nikate tamaa kabisa ya maisha,Mungu amenijaalia watoto wawili wa kike,lakin baada ya kujifungua mtoto wangu wa kike ,niliugua sana hali iliyopelekea kutolewa kizazi kutokana na kizazi kuwa na uvimbe mkubwa,baada ya hali yangu kuwa nzuri kiafya,ndipo nilipata mawazo mapya ambayo yaliamsha upya ndoto zangu,nikaamua kwenda kutafuta kazi licha ya kuwa na elimu ndogo ,lakini sikukatishwa tamaa na hilo,mwaka 2014 nikapata kazi kwenye shirika la SHDEPHA+ chini ya ufadhili wa WRP ,ni kawa kama volunteer (peer educator) ambao tulikuwa tunatoa elimu mbali mbali,zinazohusu kujikinga na maambukizi ya virus I vya UKIMWI,MILA NA DESTURI ZINAZOCHOCHEA MAAMBUKIZI YA VVU,ATHARI ZA MIMBA ZA UTOTONI ,UKATILI WA KIJINSIA NA AINA ZAKE NK. katika jamii yetu kwenye makundi rika tofauti tofauti,yakiwemo makundi ya bodaboda,wanafunzi,mama lishe ,wasichana na wanawake waliozaa katika umri mdogo nk.hapo nikapata mawazo mengi zaidi ambayo yalifanya nitambue kuwa mafanikio au malengo ya mtu yoyote yanawezekana endapo ,wewe mwenyewe utajikubali na kuamini unaweza,bila kujali wewe ni nani,umeoa au umeolewa ,Umesoma au hujasoma,nikapata mwanga mpya,hvyo nilitumia nafasi yangu kama muelimishaji rika ,wa kuhamasisha jamii yangu hasa makundi ya wanawake na watoto wa kike ambao ndio yalikuwa makundi makubwa ya wahanga kwenye jamii,changamoto nilipata sana ,kutokana na mume wangu alikuwa hataki nifanye kazi,na jamii niliyoishi nayo nilikuwa na changamoto kubwa sana hasa kuamini mwanamke anaweza akafanya jambo fulani ambalo linaweza likaleta maana kwenye jamii inayotuzunguka,pamoja na hayo yote sikukata tamaa,lengo ilikuwa ni kuionesha jamii kuwa mwanamke anaweza ,hivyo apewe nafasi,baada ya hapo nilipata nafasi kwenye kampuni ya utafiti ya Nielsen ,nilifanya kazi kama interviewer,na nilikuwa nafanya utafiti kwenye maduka yanayouza bidhaa za matumizi ya nyumbani ,na huku nikiendelea kufanya kazi kwenye shirika la SHDEPHA+ kama muelimishaji rika.Baada ya kuendelea najitihada hizo kwenye Nazi,wasichana na wanawake wengi mkoani hapa waliona mabadiliko kwangu hvyo wengi walinifuata na kuniomba niwatafutie kazi,na pia wengine walinifuata kwa ushauri ,nilijitahidi kubadilisha mtazamo wa wanawake na wasichana wengi ambao waliamini hakuna njia ya mafanikio kwa mwanamke ambae hajasoma,na pia familia yangu ilianza kunielewa kuwa inawezekana mwanamke akachangia mawazo na kulete maendeleo ndani ya nyumba,hivyo natamani sana wasichana wengi waige mfano huu kwani nimekuwa mfano mkubwa kwenye jamii yangu na nafurahia kwa mabinti wachache waliofanikiwa kupitia Mimi ,ingawa bado malengo yangu hayajakamilika,ila naamini nitafanya kitu kikubwa sana ambacho wanawake, wasichana na jamii nzima wataelewa kuwa maisha ni mtazamo na malengo ya kila mmoja wetu aliyojiwekea.

Ask CLARA MALINGUMU View Your Questions to CLARA


Image Preview

Aunt Sadaka is here for you

Who is Aunt Sadaka?      View Your Questions

About Aunt Sadaka

Aunt Sadaka is a trained counselor with over 10 years experience in councelling and coaching young girls in various issues. She is here to share with you her advice and experience. Ask her any question you may have, she will answer you and she assures you of confidentiality.

Would you like to Volunteer?

    

Request to be Kinara

    

Setting Goal